Jumapili 29 Machi 2026 - 18:00
Ujumbe muhimu wa Ayatullah A'rafi kwa wananchi makini na shujaa wa Jamhuri ya Kiislamu Iran, na Umma wa Kiislamu

Hawza/ Ayatullah A'rafi ametoa ujumbe muhimu uliowasilishwa kwa wananchi makini na jasiri wa Jamhuri ya Kiislamu na Umma wa Kiislamu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Alireza A'rafi, Mkurugenzi wa Vyuo vya Dini Iran, ametoa ujumbe muhimu uliowasilishwa kwa wananchi makini na mashujaa wa Iran pamoja na Umma wa Kiislamu.

Matini ya ujumbe huo ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mwenye kuwadhinda wenye kutakabari

“Na piganeni nao mpaka isiwepo fitna na mateso, na Dini yote iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Lakini wakiacha, basi hakika Mwenyezi Mungu anayaona wanayo yatenda.”
(Surat Al-Anfa'l: 39).

Wananchi makini na shujaa wa Iran na umma mkubwa wa Kiislamu na safu za muqawama duniani wanajua kuwa; vita ya miaka miwili iliyopita na Vita vya Ramadhani iliyozushwa na Marekani na Wazayuni ni vita vya msalaba vya kisasa na mpango wa kishetani uliozagaa ambao umelenga ustawi na uwepo wa Iran na Umma wa Kiislamu, na unalenga kukandamiza uhuru na heshima ya Iran, kuimeza Palestina na Umma wa Kiislamu, na kuwakandamiza wanaotafuta uhuru na muqawama; kwa kifupi, ni jitihada za kuleta utumwa na kuyarejesha nyuma maeneo yote katika ulimwengu wa Kiislamu.

Katika mapambano haya makubwa, fikra ya Mapinduzi ya Kiislamu na Imam mkubwa (ra) na Imam aliyeuawa kishahidi (ra), pamoja na mashahidi wa heshima, na wananchi jasiri na imara wa Iran, na mfumo wa Kiislamu ulio imara, na vikosi vya majeshi, na uongozi madhubuti wa Iran, sambamba na mataifa huru katika ukanda na mhimili wa muqawama, wamepindua mipango dhalimu na miradi tata ya mabwanyenye wa dunia wenye ulafi na wauaji na watamani wa ufisadi, na wamebadili hesabu za kimataifa. Vita vya Ramadhani ni kitovu cha kihistoria na lulu angavu katika safari ya kusimama imara, uvumilivu na mapambano yasiyo na kifani, na vimeustaajabisha ulimwengu. Sisi sote katika ulinzi huu wa kimungu na mapambano haya ya kihistoria tunalo jukumu zito.

Wajibu wetu wa kisheria, kitaifa, kiimani na kihistoria ni kusimama imara, kuwa wavumilivu na kusalia thabiti katika ahadi ya Mwenyezi Mungu, kuamini msaada wa ghaibu, na kuelekeza nguvu na uwezo wote katika kuendeleza ulinzi, kuunga mkono vikosi vya majeshi madhubuti, mfumo wa Kiislamu, uongozi mtukufu na mhimili wa muqawama. Mara'ji wakubwa wa taqlid huko Qom na Najaf na maeneo mengine, na wanazuoni wakubwa wa vyuo vya dini pamoja na taasisi za kielimu na uhakiki nchini na duniani kote, wameonesha njia na kubainisha jukumu, na wamesimama imara. Sambamba na kutoa shukrani kwa vikosi vya jeshi na wananchi, mambo yafuatayo yanakumbushwa:

1. Kuendeleza kwa ujasiri na kwa umakini mapambano na ulinzi wenye kujitoa mhanga, wa kishujaa na wa ufahamu, juu ya malengo ya Uislamu, heshima ya Iran na utukufu wa muqawama ni jukumu la viongozi wote, taasisi na vikosi vya jeshi wenye kufahamu na kujitoa mhanga nchini Iran na katika mhimili wa muqawama; na hapapaswi kuwa na uzembe hata kwa muda mfupi.

2. Kuendelea kwa uwepo wa watu na vijana wapendwa katika medani ya vita na mitaani, na kuwaunga mkono wapiganaji mashujaa, viongozi, nguzo za mfumo na uongozi ndani Iran, na vilevile kuamsha wimbi la ushirikiano wa mataifa ya eneo na wapenzi wa uhuru duniani na Uislamu, muqawama na Palestina katika ulimwengu mzima, ni mkakati muhimu unaopaswa kupewa kipaumbele na wote.

3. Umuhimu wa maandalizi kamili ya wananchi, serikali, taasisi zote, mataifa ya eneo na mhimili wa muqawama kwa chaguo lolote litakalojitokeza na kwa jihadi tukufu iliyo mbele yetu, pamoja na kuweka tayari nyenzo na mazingira yote yanayohitajika.

4. Ulazima wa kuamka kwa mataifa ya Kiislamu, wanazuoni, taasisi za kielimu na za kidini katika eneo na ulimwengu wa Kiislamu, na ushirikiano wao na upande wa haki na watetezi wa umma, lengo la Palestina, na ukombozi wa ulimwengu wa Kiislamu kutoka katika udhibiti wa Marekani na Israel.

5. Hawza, inapaswa kama ngome thabiti na kituo cha kudumu, kutekeleza jukumu lao la kihistoria, na sambamba na wananchi wakubwa wa Iran, vijana wapendwa, Basiji waheshimiwa, vikosi vya ulinzi na usalama, pamoja na viongozi waheshimiwa, wawe wachapakazi, na waendelee kwa bidii na kwa ikhlasi kutekeleza wajibu wao wa tabliigh, ufafanuzi na jihadi. Kwa sababu katika kipindi hiki kigumu cha kihistoria, wananchi wote na taasisi zote, hasa vyuo vya dini, vyuo vikuu, wasomi, wenye fikra na wanahabari, wana majukumu maalumu na maradufu; na vyuo vya dini na wanazuoni wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kujitoa muhanga na kuhudumia, na kuendelea katika njia iliyoainishwa.


“Na msaada hautoki isipo kuwa kwa Mwenyezi Mungu, Aliye tukuka, Mwenye nguvu na Mwenye hikima.”

Alireza A'rafi  
Mkurugenzi wa Vyuo vya Dini (Hawza), Nchini iran.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha